Matone ya sumu kisimani
1995 KIPINDI kilichokuwa kinaelekea Uchaguzi Mkuu kilikuwa kipindi cha kusisimua kwa wote wanaohusika kutokana na ari isiyo ya kawaida iliyodhihirishwa na washiriki wa aina mbalimbali, wakiwamo mashabiki wao, wakiwamo wagombea, wasimamizi wa shughuli za uchaguzi, wachambuzi wa masuala ya kisiasa, waandishi wa habari, wachumia-tumbo katika msako wa mradi mpya, na kadhalika. Hii ni hali ya kawaida katika vipindi kama hivi, na wala haishangazi. Nchi zote duniani ambazo zimewahi kuandaa uchaguzi…...